Tunaishi kwenye chumba kidogo katika jengo kubwa lenye ghorofa nyingi linalotoa makazi kwa familia kadhaa zinazoishi maisha ya kiwango wastani. Lakini, wanafamilia wa Felis Domestica ambao wamelipenda jengo letu hata hivyo wanaweza kukizidi kizazi cha watu wa awali cha wa jamii ya sokwe yaani ‘Homo Sapiens’. Kwa sababu wanyama hawa wenye miguu minne na walio na kucha za kufumbatika, na wanaojiringia kuwa na mabinamu wao nchini, wakiwa ni pamoja - Simba, Chui milia, Simba-mangu na Pakamwitu. Kwa kawaida, wanyama hawa hawaogopi chochote katika mazingira yao. Idadi ya wanyama wa jamii ya paka huwa na maisha marefu na hutia hofu sana na hata hivyo hutoa amani kwa wengi.
Paka hawa kwenye mtaa wetu wana alama zao za kipekee za kuweka mipaka ya maeneo. Panya wa ghorofa ya chini, ghorofa ya kwanza na ya pili hubakia kwenye ghorofa zao isipokuwa pale wanapoenda kusaka chakula huko jikoni kwenye eneo la kiusimamizi. Mtaro huo umetengwa maalum kwa ajili ya vijana na mara kwa mara hutumiwa na watawala wakuu, kutoka zamani Siam kwa kulamba miili na kuotajua. Baadhi ya paka wa kufugwa hupenda kujiburudisha kwenye vipembe vyenye kupendeza ili kukoroma na kupata usingizi mwanana na tena wakati mwingi huwa ni katika sehemu ambazo hakuna hata nafasi ya paka hao kubembea, kama vile kwenye dungu la askari gongo, mahali ambapo wangeweza kumgutusha askari huyo anapopata lepe lake la usingizi. Mungu amewabariki paka hawa na aina mbili za visanduku vya sauti, moja ikiwa ni ya kukoroma na nyingine ya mlio wa paka wa sauti nyororo. Katika eneo la makazi yetu huwafanya wenyeji wote kuwa macho na miziki ya usiku inayotumia vinanda wakati wa hafla maalum.
Baadhi ya wakazi ambao wanataka kuwa wasafi kama paka katika mtalawanda hukasirika wakati paka hao wa kijivu wanapoharibu vitu vyao. Vipanga walio miongoni mwa wakazi wanahisi kwamba paka hawa wanapaswa kufukuzwa kwa kutumia mgwisho wenye mafundo tisa. Lakini njiwa hawajaamua huku wakisubiri kuona ni wapi paka watakaporukia. Ama kwa kweli, hatujui ni nani atakayemvika paka kengele!